Wahamasishaji jamii Kisiwani Pemba wametakiwa kuendelea kuibua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Akizungumza na wamahasishaji Jamii kutoka Wilaya ya Wete na
Micheweni huko Ofisi za Pegao Chake Chake, mratibu wa Chama cha Waandishi wa
Habari wanawake Tanzania TAMWA Kisiwani Pemba Bi. Fat-hiya Mussa Said, amesema
miongoni mwa changamoto zinazopelekea wanawake wengi kushindwa kushiriki katika
nafasi za uongozi ni pamoja ukosefu wa huduma bora za Afya.
Akiwasilisha mada muhamasishaji Jamii kutoka Wilaya Micheweni
Bi. Asha Rashid Abdalla, amesema miongoni mwa changamoto walizoziibua katika
Shehia ya Kinyasini Wizi wa mifugo, mazao pamoja na vitendo vya udhalilishaji.
Kwa upande wake muhamasishaji Jamii kutoka Wilaya ya Wete
Husna Ali Said, amesema katika mkutano waliofanya na wananchi wa Shehia ya
Limbani wamegundua idadi kubwa ya vijana wakiume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia
moja, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa Jamii.
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema wakati umefika kwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuliangalia kina suala la Vijana wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja ili kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Mradi huo wa kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi
mbali mbali za uongozi, unaendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania
Tamwa Zanzibar, jumuiya ya mazingira na Utetezi wa kijinsia Pemba (PEGAO)
pamoja Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na kufadhiliwa na
Ubalozi wa Norway Tanzania.