Walimu wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa mtandao baada ya kuiba zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 200 kutoka katika benki ya Mwalimu iliyopo jijini Mwanza baada ya kuingilia mawasiliano na akaunti za benki hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amezungumza na wanahabari na kuelezea namna wizi huo ulivyofanyika na namna walivyoweza kuwanasa walimu hao wakiwa wengine wamenunua pikipiki.
BOFYA KUTAZAMA VIDEO HII KUPITIA YOUTUBE