Kuelekea siku ya wanawake duniania inayotarajiwa kufanyanyika Machi 8, 2023 , mkoani Morogoro wanawake wameanza kukutana kujadili masuala mbalimbali ya kijamii.
Miongoni mwa Mambo yaliyojadiriwa katika kongamano lililofanyika kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro wanawake hao wamesema wamechoshwa na mikopo kausha damu hivyo wanaiomba serikali kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake ili kuwaepusha na mkopo kausha damu.
Aidha wanawake hao wamesema kutokana na ugumu wa kurejesha mikopo hiyo maarufu kama mikopo kausha damu baadhi ya wanawake wamelazimika kuchepuka ili wapate fedha za kulipa mikopo hiyo.
Wanawake hao wamefafanua kuwa ndoa nyingi zipo kwenye hatari kuvunjika kwa sababu ya mikopo hiyo kwani baadhi yao wamelazimika kuuza vitu vya ndani kama Sofa,Tv,Redio na Godoro ili wapate fedha za kurejesha.
Mikopo hiyo inayotolewa na taasisi binafsi inamashariti ambayo humlazimu mkopaji kurejesha fedha hizo kila siku kulingana na kiasi cha mkopo uliochukua.
KAMA HUJATAZAMA VIDEO HII TAZAMA SASA