Wanawake wawili wanaswa na swala

0

 Wanawake wawili wa Kijiji cha Kimana wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kiteto kwa kukutwa na nyara za Serikali, ambazo ni Swala na mtoto wa mnyama aina ya Digidigi ambaye yuko hai.Wanawake hao ni Veronica Paulo (24) na Witnes Paulo (20) ambapo Machi 20.2023 wakiwa nyumbani kwao wamedaiwa kukutwa nya nyara hizo za Serikali wakiwa eneo la Njutaa kata ya Partimbo.

Afisa Maliasili Wilaya ta Kiteto, Doris Gama ametaja thamani ya mnyama aliyeuawa aina ya Swala kuwa ni dola za Kimarekani 35 sawa na sh 77,000 elfu za Kitanzania Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amethibitisha tukio na kudai kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top