Na, Hassan Msellem.
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa Kusini Pemba kwa tuhuma za kumshambulia na vitu vyenye ncha kali Maulid Haroub Mpemba miaka 45, ambaye ni mfanya bishara wa miamala ya kifedha na wakala wa Banki ya watu wa Zanzibar PBZ mkaazi wa Makaange Kengeja Wilaya ya Mkoa wa Kusini Pemba.
Tukio hilo limetokea March 17.2023 majira ya saa 9 alfajiri
huko Makaange Kengeja nyumbani kwa Ngudu Maulid Haroub Mpemba.
Akizungumza na Idawaonline.com Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kusini Pemba Kamishna msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa alisema “Mnamo tarehe 17.03.2023 majira ya saa 9
alfajiri huko Makaange Shehia ya Kengeja Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba,
watuhumiwa wasiojuilikana walivunja mlango wa nyumba ya bwana Maulid Haroub Mpemba
mwenye umri wa miaka 45 Mkaazi wa Makaange kumshambulia na vitu vyenye ncha
kali nab utu sehemu mbali mbali za kichwa chake chanzo cha tukio hilo bado
kinachunguzwa kujua sababu ya kumjeruhi huyu muhanga baada ya tukio hilo
watuhumiwa watatu walikamatwa kwa ajili ya mahojiano ambao ni Saleh Mohammed
Abdalla maarufu Bambe miaka 33 mkaazi wa Mjiweni Kengeja, Salum Mohammed Seif
maarufu Rumbwi miaka 46 mkaazi wa Tumbi Shehia ya Chumbageni na Mohammed Rashid
Mohammed miaka 42 Mkaazi wa Mjiweni Kengeja”
Aidha Kamanda Abdalla, ametoa wito kwa wananchi kutii Sheria bila ya shuruti na kutokujichulia sheria mkononi.
Akikiri kupokelewa kwa Majeruhi huyo daktari dhamana wa
hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Rashid Saleh Hemed, alisema “Ni kweli tarehe 17.03.2023 majira ya saa 11:30
alfajiri tulimpokea ndugu Maulid Haroub Mpemba miaka 45 mkaazi wa Makaange
Kengeja akiwa ameruhiwa sehemu mbali mbali kichwani majeruhi huyo alipatiwa
matibabu lakini baadae tuliamua kumsafirisha kumpeleka hospitali ya Mnazi Mmoja
kwa ajili ya uangalifu zaidi.