Wawili Kiteto wanusurika kifo kwa kupigwa risasi

0

 Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kupigwa na risasi aina ya gobole na majangili wanaosadikika kwa ni wezi wa mifugo katika Kijiji cha Makame wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amewataja majeruhi hao kuwa ni Philipo Meleki (67) na Lazaro Philipo (35) ambapo alisema tukio hilo limetokea Machi 8,2023 katika Kijiji cha Makame Manyara saa mbili usiku wakati wawili hao wakikagua mifugo kwenye makazi yao yaliyokuwa eneo la hifadhi ya WMA Makame.

"Tukio hili lilitokea usiku saa mbili na inasadikiwa waliofanya tukio hili ni majangili waliokuwa na bunduki aina ya gobole, Philipo alijeruhiwa na risasi mgongoni na Lazaro Philipo mkononi"

BOFYA KUTAZAMA VIDEO HII
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top