Aliyetuhumiwa kukutwa na sehemu za siri 5 za wanawake aachiwa huru

0

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemfutia kesi na kumwachia huru mshtakiwa Salum Nkonja (23) maarufu kama Emmanuel Nkonja, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya kukutwa na vipande viwili vya mafuvu ya kichwa cha binadamu pamoja na sehemu za siri tano za mwanamke baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa zaidi ya mara tano bila kuendelea na ushahidi.


Umauzi huo umetolewa  Jumatatu, April 17, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemalira wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 32/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Mbali na kumfutia mashtaka na kumwachia huru, mshtakiwa huyo, Mahakama hiyo imeamuru mshtakiwa asikamatwe mpaka upande wa mashtaka watakapowasilisha vielelezo mahakamani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top