ANUSURIKA KIFO KWA KIPIGO KISA WIZI WA KUKU

0

Taharuki imezika baada ya kijana aliyefahamika kwa jina la Isamail Hassan mkazi wa Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani kunusurika kifo kwa kipigo baada ya kukamatwa kwa kosa la kutaka kuiba kuku 11 ambao tayari alishawachinja majira ya usiku.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mtaa wa Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani Fadhili Chala mkazi wa mtaa huo alisema kuwa kumekuwa na wizi unaoendelea katika mtaa huo lakini walikuwa hawajapata uhakika nani anafanya vitendo hivyo.

Alisema kuwa kijana huyo alivamia nyumba na kuvunja banda na kuchinja kuku 10 akiwa anamalizia wa 11 alikutwa na wenyewe hivyo akakimbia.

“Huyu dogo tunaishi naye hapa mtaani tulikuwa tunamuhisi kuwa ni mwizi lakini tulikuwa hatuna uhakika ni mgeni anaishi na kaka yake amekuja hivi karibuni lakini tulipoamua kumfatilia tulibaini kuwa mtaa aliotoka alikufukuzwa kwa wizi hivyo tukaanza kuwa makini nae.”

“Baada ya kujua kuwa ameonwa na mwenye kuku alikimbia lakini alisahau kiatu kibaya zaidi mguu wake tunaujua hivyo ikatulahisishia kumfata na tulipomuuliza alikiri kuiba na kwenda kuwauza”

Naye Getruda Nyagari makazi wa magomeni kwa mtawike (aliyeibiwa) alisema kuwa nikiwa nimelala nilisikia kuku wanalia bandani nikaona sio kawaida ikabidi nitoke nje ambapo nilimuona mwizi akiwa kashika kuku na kisu mkononi.

“Nilipoona ameshika kisu nilirudi ndani haraka kwakujihami nikajifungia na kuanza kuita mwizi nikiwa ndani majirani waliposikia walitoka nje na mimi nikatoka nje na kuanza kumsaka mwizi huyo ambaye tayari alikuwa ameshaaondoka eneo lile na alikuwa amewachinja kuku 11 tayari kwenye karo” alisema Nyagari

Kwa upande wake mwizi mwenyewe kabla hajapelekwa Polisi, Issmail Hassan alikiri kufanya wizi huo kisha kwenda kuuza kuku hao ili apate riziki.

“Ni kweli nimechinja kuku ambao sio wangu kwa hiyo mimi ni mwizi sirudii tena yaani nimepigwa sana naomba mnisamehe nikirudia mnifanye chochote ila wizi nimeacha kuanzia leo usiku nilikuwa na pita tu nikakuta kuku nikachukua na kuchinja kuku saba tu” alisema Hassan.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top