ASAKWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE CHATO

0

Jeshi la polisi Mkoa wa Geita linamtafuta Mwanaume mmoja (jina linahifadhiwa) mkazi wa Kijiji Cha Chikorikola kata ya Mganza wilayani Chato kwa tuhuma za kuumua mkewe anayefahamika jina la Kasaka January (42) kwa sababu za wivu za mali alizokuwa anamiliki.
Picha kutoka Maktaba

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi (ACP), Safia Jongo amesema mwanamke alikuwa akimiliki mali nyingi kuliko Mwanaume na tamaa za Mwanaume zikampelekea kuwaza kumuua mwanamke Ili yeye awe mmiliki wa mali hizo.

"Mwanaume alikuwa na umri wa Miaka 56 hajabahatika kuzaa na huyu mwanamke Ili walikuwa wanaishi pamoja.

"Kabla ya mauaji hayo kulitokea wizi wa betri za sola 40 zinazotumika kwenye uvuvi nyumbani hapo wanapoishi, mama mwenye Mji (marehemu ) alikuwa anamwambia mumewe kuwa betri zangu zimeibiwa na mwizi namjua.

Ameeleza, Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta na kuwaomba ndugu kuwa watulivu na uvumilivu kuwa mhalifu huyo atapatakana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top