Ashauriwa amfanyie maombi mumewe aliyembaka mtoto wao badala ya kumshitaki

0

Mwanamke katika kaunti ya Mombasa huko nchini Kenya ameshangaza wengi kwa kukataa kumripoti mume wake ambaye alimnajisi binti yao mwenye umri wa miaka mitatu. 


Mjomba wa mtoto huyo Joseph Kithi anadai kuwa maskini mtoto huyo alinajisiwa na baba yake mzazi siku ya Ijumaa, Machi 31 nyumbani kwao Bamburi, kaunti ya Mombasa. 


Lakini juhudi za kumtaka mama yake huyo kuripoti kisa hicho kwa polisi ziligonga mwamba. Kulingana na Kithi, mwanamke huyo amedinda kumchukulia mumewe hatua akisema kwamba akimripoti mumewe atakosa mtu wa kumlisha pamoja na wanawe. 

Kithi aliongeza kuwa mshukiwa alimnajisi mtoto huyo bafuni alipokuwa akimuosha. "Siku iliyofuata mtoto huyo alianza kulalamikia maumivu kwenye sehemu zake za siri na alipohojiwa na mama yake alikiri kunajisiwa na baba yake alipokuwa akimwogesha. Baadaye alimtishia asiseme neno lolote kwa mama yake," Kithi alisema kama alivyonukuliwa na K24. 


Mama wa mtoto huyo alisema kuwa bado hajampeleka mtoto wake hospitalini kwa kuwa mshukiwa ndiye mlezi pekee wa familia. Mama wa mtoto huyo alisema kuwa bado hajampeleka mtoto wake hospitalini kwa sababu mshukiwa ndiye anategemewa kuchuma riziki katika familia hiyo. "Ni kweli ila naogopa endapo nitamripoti polisi hakuna mtu wa kulea familia yangu. 


Nilijifungua kwa upasuaji na kwa sasa siwezi kufanya kazi. Hiyo ndiyo sababu pekee inayonifanya kumvumilia mtu huyu," alibainisha. Mwanamke huyo aliongezea kuwa alishauriwa kumwombea mumewe badala ya kumripoti kwa polisi. "Siwezi kuongea kwa muda mrefu kwa sababu nilitoka kanisani baada ya kunipigia simu. Ninahudhuria ibada kwa sasa. Nimekuja kumwomba Mungu atoe pepo waliomfanya atende kendo hicho," alisema kabla ya kukata simu. simu yake.


Mtoto huyo ambaye kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa bibi yake hana uwezo wa kudhibiti mkojo wake ana uchungu mwingi kwani hakuna matibabu yoyote aliyopata. Hakuna mtu aliyekamatwa kufikia sasa kuhusiana na kisa hicho na pia hakuna ripoti rasmi iliyotolewa na jamaa wa mtoto huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top