Askofu Asimamisha Ibada baada ya viongozi wa upinzani kuhudhuria ibada

0

 Kumetokea sintofahamu Jumapili, Aprili 2,2023 baada ya askofu wa Kanisa la AIPCA Ruiru, Kaunti ya Kiambu kusitisha ibada kutokana na kuwepo kwa viongozi wa Azimio La Umoja. 

Miongoni mwa vinara wa Upinzani waliofika katika kanisa hilo ni pamoja na Martha Karua, Kalonzo Musyoka, Eugene Wamalwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna.

 Duru zinaarifu kuwa askofu huyo alisimamisha ibada na kuwaita viongozi hao pembeni ili kukubaliana ujumbe ambao watatoa kanisani. 

Inasemekana kwamba askofu huyo aliwaonya wanasiasa hao dhidi ya kuzungumzia maandamano makubwa ya Aprili 3.2023. 

Kinara wa Upinzani Raila Odinga hata hivyo, hakuhudhuria ibada hiyo na vile vile haijabainika iwapo majedari wake walikuwa wamearifu kanisa hilo kuhusu ziara yao.

 Lakini kwa mujibu wa kurasa zake za mitandao ya kijamii, katika taarifa yake mwisho, Raila alisema kuwa yuko tayari kwa maandamano makubwa ya kupinga serikali kesho.

"Sote tuko tayari na tumejiandaa kwa Jumatatu kubwa," Raila amesema kupitia mtandao wa Twitter. 

Mnamo Jumamosi, Machi 1, kwenye hafla ya shukrani iliyojumuisha zaidi ya makanisa 40 katika Shule ya Msingi ya Silungai, eneo bunge la Malava, Kaunti ya Kakamega, Raila aligeuzwa kiini cha mahubiri.

 Hafla hiyo ilihudhuriwa vigogo wa kisiasa wa Kenya Kwanza akiwemo Naibu Rais Gachagua, Kiongozi wa Mawaziri Musalia Mudavadi, na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula. 

Gachagua alitumia fursa hiyo kumshambulia Bw Odinga, akimtaja kuwa kiongozi mwenye uchu wa mamlaka ambaye huwa hatosheki hata kidogo kila matokeo ya uchaguzi mkuu yanapotangazwa. 

Naibu Rais pia alitoa onyo kali kwa waandamanaji, akiwaambia kuwa Jumatatu ndiyo siku yao ya mwisho kuandamana. Naibu Rais alisema serikali itakuwa macho Jumatatu kuwalinda wafanyabiashara na mali yao. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top