Auawa kikatiri, atobolewa macho na sehemu za siri

0

 Mwanaume ambaye hajafahamika jina amekutwa ameuawa na watu wasiojulikana huku sehemu zake za siri na macho zikiwa zimetobolewa.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Wilbrod Mtafungwa.

Mwili wake umekutwa umetelekezwa katika eneo la uwanja wa ndege pembezoni mwa kilabu cha pombe kilichopo Kata ya Misheni wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Wilbrod Mtafungwa, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili huo umehifadhiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, ukisubiri ndugu kuutambua.

Alisema mpaka sasa jumla ya watu watatu wamekamatwa kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Juzi, baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliiomba serikali kuwatafuta wahusika na kuhakikisha wanachukuliwa hatua stahiki ili kudhibiti vitendo hivyo wilayani humo.

Mchungaji James Bukwiba alisema wanaofanya vitendo hivyo wanatakiwa kuacha na kumrudia Mungu na kuwasihi wananchi kuwa na upendo na kulindana.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Misheni, Joseph Protas alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, lilitokea usiku wa kuamkia juzi na kuahidi kuendelea kufanya uchunguzi ili kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Happyfania Damian pamoja na Diwani Francis Mbungai kwa pamoja wamelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuendelea kuwa walinzi wenyewe kwa wenyewe, ili kudhibiti vitendo hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top