Baba adaiwa kumchoma mikono mwanawe kwa maji ya moto

0

 Baba mzazi anyefahamika kwa jina la Mathias Daudi, mkazi wa kijiji cha Nyarugusu, wilaya ya Geita, amedaiwa kumchoma mtoto wake kwa kuingiza mikono yake kwenye sufuria ya maji ya moto iliyokuwa jikoni kwa madai ya kuiba Sh. 5,000 kwa jirani.


Mtendaji wa Kata ya Nyarugusu, Lusekelo Mwaikenda, akielezea tukio hilo jana, alisema lilitokea Aprili Mosi, mwaka huu, majira ya saa 1:00 jioni.

Alimtaja mtoto huyo kuwa ni Elizabeth Mathias (10), mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Zahanati, Nyarugusu.

Mwaikenda alisema baada ya mtoto huyo kuiba fedha hiyo, alimpelekea baba yake akimwambia ameiokota na kisha kupangiwa matumizi ya familia.

“Mtoto huyo alipokwenda kununua vitu vya matumizi ya nyumbani kwa pesa hiyo, aliporudi nyumbani alimkuta jirani yao akimsema kuwa amemwimbia Sh. 5,000, ndipo baba yake mzazi akaanza kumtembezea kichapo na kisha kumloweka mikono yake yote miwili kwenye sufuria yla maji ya moto iliyokuwa jikoni,” alisema Mwaikenda.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Alex Herman, alisema baada ya kupata taarifa za mtoto huyo kufanyiwa ukatili na baba yake, walimfuatilia kwa ukaribu na kisha kumkamata na kumpelekea polisi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

“Tunaishukuru timu ya wanasheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa kutoa elimu ya kutoa taarifa za ukatili kwa mabaraza ya kata, ndiyo hao walitoa taarifa juu ya tukio la mtoto huyu na pia LEAT wamemtoa mtoto huyo Nyarugusu na kumleta hapa Hospitali ya Mkoa wa Geita na anaendelea kupatiwa matibabu,” alisema Herman.

Pia alisema mtoto huyo akipona hawatamrudisha nyumbani kwa baba yake, bali watamtafutia mahali pengine pa kuishi ikiwamo kwenye nyumba za kulea watoto kwa sababu tayari ameshaathirika kisaikolojia.

Ofisa wa LEAT, Valeria Macha, alisema walipokea taarifa juu ya tukio la mtoto huyo kuchomwa maji ya moto, ndipo wakawasiliana na Maofisa Maendeleo wa Geita na walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto akiwa katika hali mbaya ndipo wakamchukua na kumpeleka Hospitali ya Mkoa Geita kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Sophia Jongo, alisema taarifa za tukio hilo bado hajazipata kwa sababu yuko nje ya ofisi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top