Mwanaume mmoja Aliye fahamika Kwa Majina ya Elias Bakumye(32)mkazi wa kijiji cha Chikobe kata ya Butundwe Wilaya na Mkoani Geita,anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kutuhuma za kumuua Mtoto wake (5) Mwenye ulemavu baada Ya Yeye na Mama wa mtoto huyo kutengena na Kuachiwa mtoto amlee.
Kamanda Wa Polisi wa Mkoa huo,Safia Jongo,amesema mtuhumiwa huyo amekili kuhusika na Mauaji hayo na Kusema chanzo kilicho pelekea kufanya tukio hilo ni kushindwa Malezi ya mtoto huyo Mwenye ulemavu aliyekuwa akihitaji kupewa huduma zote.
Imeelezwa Baba huyo baada ya Kukataliwa aliondoka na Mtoto wake kurudi Nyumbani Wakati wakiwa Njiani ndipo akatekeleza Tukio hilo na Kisha kumufukia mtoto wake.