Baba Amtelekeza mkewe hospitalini baada ya kujifungua mtoto wa kike

0

 Mwanaume mmoja ametoa kali baada ya kuingia mitini pale aliposikia mkewe amejifungua mtoto wa kike huko Lagos Nigeria.


Lagos. "Kuwa na watoto wote wa kike si kosa la mwanamke" haya ni maneno ya aliyekuwa nesi wa zamu hospitalini hapo baada ya mwanaume kumtelekeza mke wake kwa sababu alijifungua mtoto wa kike wa pili mfululizo.

Muuguzi na mkunga huyo wa Lagos, aliyetambulika kwa jina la Kaykay, amesimulia jinsi mtu huyo alivyomtelekeza mkewe huku akionyesha kushangazwa na tukio hilo kuwa kuna watu bado wana imani potofu namna hiyo.

“Siamini siku hizi baadhi ya wanaume wa Kinigeria bado hawajui kuwa na watoto wote wa kike si kosa la mwanamke, hivi ndivyo mwanaume huyu hajafika kumuona mke wake hospitali tangu atoke kujifungua siku tatu zilizopita kwa sababu alikuwa na mtoto mwingine wa kike,” aliandika kwenye Twitter Ijumaa, Machi 31.

Inasemekana baba huyo alikuwa na matarajio ya kupata mtoto wa kiume lakini alikerekwa na taarifa kuwa wamepata tena msichana, tovuti ya LindaIkeji ya Nigeria imeripoti tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top