Baba atuhumiwa kumuua binti yake aliemfuma akitaka kufanya mapenzi

0

 Binti mmoja ajulikanae kwa jina la Milembe Mihayo mwenye umri wa miaka kumi na moja mkazi wa Kitongoji cha Ishungi wilayani Kwimba mkoani Mwanza, amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya hiyo akiuguza majeraha mbalimbali kwenye mwili wake baada ya kupokea kipigo kutoka kwa baba yake mzazi.


Inadaiwa kuwa binti huyo alikutwa na baba yake akiwa bafuni na kijana mmoja wakiwa wamevua nguo wakitaka kufanya mapenzi kitendo ambacho kilimkera baba yake huyo aitwaye Mathayo Mishaka ndipo akaanza kumchapa na fimbo huku kijana aliyekuwa naye akifanikiwa kukimbia

Aidha baada ya kupokea kichapo cha fimbo binti huyo alizidiwa na kukimbizwa hospitali ndipo akapoteza Maisha, hadi sasa baba huyo Mathayo Mishaka anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha binti yake huyo

Kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya Habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutoa adhabu za kikatili kwa watoto wao badala yake watumie njia sahihi ya kuwaonya pindi wanapokose ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top