Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumlewesha pombe na kumuingilia kimwili binti yake wa kufikia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mwanaume huyo kuwa ni Mseveni anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 hadi 40.
Kamanda Magomi amesema binti aliyekumbwa na madhila hayo ana umri wa miaka 12 na ni mwanafunzi wa darasa la Saba katika shule moja mkoani humo.
“Katika hili jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga hatutakuwa na mhali kwa mtuhumiwa kwani kitendo alichofanya sio cha kiungwana haiwezekani baba kubaka mwanae tutahakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwake ili iwefundisho kwa watu wengine "alisema Kamanda Magomi.