DC atoa siku 14 waliopiga Mil. 100 kuzirejesha

0

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame ameitaka TAKUKURU Wilaya ya Gairo kuchukua hatua kwa watumishi na watu wengine waliohusika katika vitendo vya rushwa na kupelekea fedha za Halmashauri ya Gairo zaidi ya Milioni 100 zilizokopeshwa katika kipindi cha Mwaka 2020 hadi 2023 kutorejeshwa, kutokana na uzembe na zingine kukopeshwa vikundi hewa.


Aidha, ametoa siku 14 kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuja na Mpango wa namna fedha hizo zitavyorejeshwa mikononi mwa Serikali ili wananchi wengine waendelee kukopeshwa, sambamba na kumtaka mkaguzi wa ndani kujenga utamaduni wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepuka dosari hizo.

Hayo yamebainishwa katika kikao Kazi kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa lengo la kupokea taarifa ya Tathmini ya Utoaji wa Mikopo katika kipindi Cha Miaka 3 iliyopita.

Taarifa hiyo ilitokana na Kamati iliyoundwa mwezi Februari na Kamati ya Usalama Wilaya ya Gairo kuchunguza Mwenendo wa Utoaji na urejeshaji Mikopo ya Vikundi ambapo miongoni mwa dosari zilizobainika na Kamati hiyo ni pamoja na uwepo wa Vikundi hewa, baadhi ya Vikundi kupokea fedha na kugawana bila kufanya miradi kusudiwa, ukiukwaji wa taratibu wa Utoaji wa mikopo pamoja na kukosekana kwa tija ya mikopo hiyo kwa walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo ndugu Dastan Daudi Mwendi alieleza lengo la kutoa mikopo hiyo ni kuwawezesha wananchi kiuchumi hivyo kukijengea heshima Chama Cha Mapinduzi. Aliitaka Halmashauri ya Gairo kusimamia urejeshaji wa fedha hizo haraka iwezekanavyo.

Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Bi Msifwaki Haule alieleza tayari Halmashauri ilianza kufanyia kazi Changamoto hizo za vikundi na kwamba ripoti iliyotolewa itawasaidia zaidi juu ya maeneo muhimu ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top