Serikali Wilayani Pangani imepanga kushirikiana na Uongozi wa Madereva Bodaboda kuanzisha SACCOS ambazo zitakuwa ni kama VICOBA ambapo Serikali, Bodaboda na Viongozi wataweka fedha zao lengo likiwa ni kuinua vipato vya Bodaboda na kuhakikisha kila Dereva Bodaboda anamiliki pikipiki yake mwenyewe.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa Uchaguzi wa Viongozi wapya wa Bodaboda Pangani, DC wa Pangani, Zainab Abdallah @zainababdallah93 amesema “Uongozi ukipatikana tukae chini tuunde SACCOS ya Bodaboda Pangani ambayo itakuwa kama VICOBA, nyinyi Wanachama mna uwezo wa kuchangia mule, Serikali ikipata fedha inaweza kuleta mule, Viongozi na Wadau wa maendeleo wakipata wanaweka mule"
"Tufanye makadirio tu hapa Bodaboda Wilaya tupo 1000 mkisema kwa siku muwe na uwezo wa kuchangia Tsh Elfu moja maana yake kwa mwezi mnaweza wa kupata Milioni.30, haiwezekani asilimia kubwa ya Madereva Bodaboda, Bodaboda hizo ni mali za Watu wengine lazima kuwe na malengo ya kuhakikisha wote mnamiliki Bodaboda zenu wenyewe"
"Mkiweka utaratibu mzuri wa kuchanga iwe kila siku au kwa Wiki na sisi Serikali tukawapa support mtafika mbali, leo nataka niahidi Mimi binafsi nitawachangia Mil 5 kwenye hiyo SACCOS"
"Mbunge wenu wa Pangani ambaye ni Waziri wa Maji (Jumaa Aweso) alifanya harambee hapa akachangisha Tsh.Mil 65 ameniambia utaratibu wa SACCOS ukikamilika tutaingiza zile pesa kule, zile pesa sio kwa ajili ya Watu kujinufaisha na Familia zao, umekuwa Katibu hela tumeingiza unaanza kumiliki gari, tunaingiza pesa ili Bodaboda wa Pangani wamiliki pikipiki zao wenyewe"