DC wajawazito sasa sitisheni kutumia mitishamba,,,Njooni kwenye zahanati yenu

0

Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wanawake wilayani humo kuacha tabia ya kunywa dawa za mitishamba pindi wanapokuwa wajawazito na badala yake waende hospitali ili kupata huduma sahihi na hatimaye wajifungue Watoto wenye afya.


Ludigija ametoa kauli hiyo wakati akizindua huduma za afya katika zahanati ya Sangu iliyopo katika Kijiji cha Sangu kata ya Mhande na kuwataka wakazi wa Kijiji hicho kutunza miundombinu ya zahanati hiyo ili iwasaidie kupata huduma za afya.

Niwasihi wananchi inawezekana mmesubiri kwa muda mrefu kupata zahanati hii sasa mmepata itumieni vizuri wataalamu wa afya wapo niwaombe mtoe ushirikiano kwao na hasa wanawake hatutarajii kusikia mnajifungulia nyumbani mana huduma imesogezwa karibu vilevile achene kutumia dawa za mitishamba mkiwa wajawazito maana ni hatari kwa mtoto aliyepo tumboni’

Katika hatua nyingine Dc Ludigija amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanalala kwenye chandarua ili ili kujikinga na ugonjwa wa maralia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top