Siku ya Alhamisi, March 30,2023 familia moja ilitupa jeneza ambalo mkwe alinunua kwa ajili ya mazishi ya mama mkwe wake.
Mtumiaji wa Facebook, Bem Raphael Aondongu, ambaye alishirikisha kisa hicho, alisema tukio hilo lilifanyika Tombo Mbatie, katika eneo la Buruku katika jimbo la Benue.
Bem alisema watoto wa marehemu walikataa jeneza hilo kwani familia iliona si zuri na la bei rahisi kutumiwa kwa marehemu mama yao.
Akielezea kuhusu mila ya TIV iliyomlazimu mkwe kupeana jeneza, Bem aliandika:
“Kama mila ya TIV inavyodai, mama au baba anapofariki, mtoto wa kwanza wa kike ambaye ameolewa ndiye anayebebeshwa jukumu la kuandaa jeneza kwa ajili ya mazishi ya mzazi yeyote kati ya waliofariki.
“Na kwa ajili ya kudumisha mila, mtoto wa kwanza wa kike kwa kushirikiana na mumewe ambaye ni mkwe wa marehemu mama, walijaribu kadri ya uwezo wao kuleta jeneza hili kwenye picha lakini lilikataliwa.
Maoni ya watu kuhusu kioja hicho; Pretty Doo alisema: "Kusema ukweli huu ni udhalilishaji, je kwani mfu alimkosea kwa njia yoyote ile? "Ingawa maisha tayari yamepotea na sanduku haijalishi lakini ukweli hata kama ni mimi sitakubali."
Malkia Terlumun Doowuese Jennifer alisema: “Mama mkwe wangu alipofariki dunia na mdogo wa mume wangu kutakiwa kununua sanduku, hwakuwa na hela za kutosha kutengeneza ndipo mume wangu akaamua walete wanachomudu kwa wakati ili familia iongeze pesa na tengeneza sanduku."