Hakimu kizimbani kwa rushwa ya Tsh 5,000

0

 Hakimu Mkazi wa Mtwara, Mussa Esanju amefikishwa Mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoa wa Mtwara, kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Shilingi 50,000 kutoka kwa mtuhumiwa.


Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mtwara, Lucas Jang’andu, Hakimu Mussa amesomewa makosa mawili ya ushawishi wa kuomba fedha shilingi 200,000 na kupokea shilingi 50,000.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara, Enock Ngailo amesema Mtuhumiwa alikamatwa Aprili 5, 2023 Mangamba Tanki la Maji, akiwa na fedha za mamlaka hiyo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji.

Hata hivyo, baada ya kusomewa shitaka mtuhumiwa amekana na kuachiwa kwa dhamana na kesi hiyo itatajwa tena May 18, mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top