Hati ya pamoja inasaidia kuepusha ukatili kwa wanawake

0

Imeelezwa kuwa umiliki wa pamoja unaweza kumsaidia mwanamke katika kumkwamua kiuchumi kwani endapo mwanamke atashirikishwa katika umiliki wa ardhi itasaidia kuweka ulinzi wa mali hiyo.

Augustino Mchami ni msaidizi wa kisheria kutoka kituo cha msaada wa kisheria njombe amesema kuwa umiliki wa pamoja unasaidia katika kuweka ulinzi wa mali za familia kwani kwa kuwepo ushirikishwaji huu husaidia kuondoa udanganyifu wa mali .

amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwepo kwa ulinzi kwa mwanamke ambapo ana haki ya kutumia mali za mumewe kwa ustawi wa familia pia ana haki ya kuweka rehani mali ya mume ambayo wamechuma pamoja ili kutatua tatizo linalokuwa limejitokea kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

kwa upande wake Sara Magehema ambaye pia ni msaidizi wa kisheria njombe amesema wanawake bado wapo kwenye janga la kutomiliki ardhi kutokana na utamaduni uliojengeka tangu zamani na kwamba mfumo huu bado upo mpaka sasa.

Amesema kwa sasa zama zimebadilika na mwanamke pia ana haki ya kumiliki ardhi hivyo amesema kuwa elimu zaidi iendelee kutolea kwenye jamii ili kutambua mchango wa mwanamke na yeye aweze kumili ardhi.

Hata hivyo mkurugenzi wa kituo cha msaada wa kisheria njombe Geofrey kaduma amasema umiliki wa pamoja utasaidia kuweka ulinzi wa mali za familia hata ikitokea mmoja kati ya mwanamke au mwanaume amepoteza maisha mali za familia zinakuwa katika mikono salama tofauti na pale mtu angefanya siri kuhusu mali zake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top