Idadi ya watu nchini India, inatarajiwa kupita ile ya China

0

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na idadi ya watu, inakadiria kuwa kufikia mwisho wa mwezi Juni, India itakuwa na watu Bilioni 1 Milioni 4, Laki Mbili na 86, na kuizidi China ambayo itakuwa na watu Bilioni 1 Milioni 4, Laki Mbili na 57.

Hii imekuja baada ya mwaka uliopita, idadi ya watu nchini China kupungua kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1960, huku India ikiendelea kushuhudia ongezeko la watu.

Wakati India, inapotarajiwa kuongoza kwa idadi ya watu duniani, kuna wasiwasi kuwa idadi kubwa ya raia wake bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ukosefu wa umeme, chakula, na makaazi mazuri.

Aidha, mitaa ya mabanda yenye watu wengi katika baadhi ya miji inatarajiwa kuendelea kuongezeka kutokana kutokuwepo kwa mpangilio mzuri wa makaazi.

Tangu mwaka 2011, India haina takwimu kamili ya idadi ya raia wake, baada ya kushindwa kufanikisha zoezi la sensa la mwaka 2021 baada ya kuzuka kwa janga la Uviko 19.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top