Idadi ya waumini waliokufa kwa kufunga yaongezekana nchini Kenya

0

Mnamo Jumapili, Aprili 23, makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamefukua miili 18 zaidi katika Msitu wa Shakahola, Kilifi, inayoaminika kuwa ya wafuasi wa mchungaji tata Paul Mackenzie.

Miili sita ilipatikana kwa mara ya kwanza kwenye makaburi matatu yenye kina kirefu. Saa chache baadaye, miili 12 zaidi ilipatikana katika makaburi saba, na hivyo kuongeza idadi ya mateka wa mchungaji huo kufikia 39.

Mmoja ya waumini wa Mackenzie alikataa chakula Wakati wa zoezi la ukozi, wapelelezi walimuokoa mwanamke mmoja ambaye anasemekana alikuwa katika hali mbaya kiafya.

Hata hivyo, mwanamke huyo aliwashangaza wapelelezi na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu akionyesha ishara kwamba hataki kutibiwa.

Wakati maafisa wa afya walipojaribu kumpa maji yaliyochanganywa na sukari ili kumpa nguvu, mwanamke huyo alikaza mdomo wake kwa nguvu.

Mwanamke huyo aliyekuwa hoi, alionyesha ishara kwamba hataki kutibiwa bali aachwe afe.

Hata hivyo, maafisa wa afya walimweka kwa nguvu mwanamke huyo kwenye gari la wagonjwa na kumkimbiza katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Malindi kwa matibabu zaidi. 

Pasta Mackenzie akataa chakula gerezani Awali, iliripotiwa kwamba mtumishi wa Bwana mwenye utata Paul Mackenzie kutoka kanisa la Good News International amekataa kula chakula akiwa gerezani.

Mackenzie anazuiliwa baada ya kutuhumiwa kuwa aliwashawishi washirika wake kufunga kula hadi kufariki dunia.

Ripoti ya polisi inasema Mackenzie amekuwa akikataa kula wala kunywa chochote tangu alipokamatwa kuhusiana na vifo vya washirika wake.

Makachero walisema kwa wakati mmoja walitaka kumpa kikombe cha maji lakini akagoma akisema ni wakati wa kufunga na kuomba.

Kwa mujibu wa baadhi ya jamaa wa familia za walioathirika, wanansema kanisa hilo huwataka watoto kuanza kufunga hadi kufariki, kisha wanafuatwa na kina mama na mwisho wanaume.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top