JESHI la Polisi Mkoa wa mwanza limesema kwamba mnamo Aprili Mosi muda wa saa 20:00 Usiku huko kitongoji cha Kasuzu, kijiji na kata ya Namagondo, tarafa ya Mumulambo wilayani Ukerewe, mwanaume aitwaye Anselumu Sebuka, miaka 42, Mkulima na mkazi wa Namagondo, alikutwa ndani ya chumbachake akiwa amejaribu kujiua kwa kukata uume wake kwa kutumia kisu chenye ncha kali.
Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Wilbroad W. Mutafungwa- SACP imesema kuwa inadaiwa Ansele Sebuka alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake kuiba mali mbalimbali za familia yake na za jamii inayomzunguka na kwenda kuziuza pamoja na ulevi uliokithili ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia zake mbaya.
Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kisu na kuacha unaning’inia kwa lengo la kujiua, Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliopelekea mhanga kupata msongo wa mawazo.
Ansele Sebuka alipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata njia sahihi za kutatua matatizo yao hususani kuwaona wataalamu wa afya ya akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa mawazo na kukosa uvumilivu wa migogoro mbalimbali katika jamii.