Jela miaka 30 kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

0

 Mahakama ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela Claud Mwinuka (22) maarufu kama ‘Kibakuli’ baada ya kukiri kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.


Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Paul BarnabasAlhamisi 6, 2023 baada ya mtuhumiwa kufikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Amesema Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kukiri kosa la kuruhusu kuingilia kinyume na maumbile na wanaume, huku akijua ni kosa la kifungu cha 154 kifungu kidogo cha kwanza (C )cha sheria ya kanuni ya adhabu kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Hakimu Barnabas amesena wametoa hukumu kwa mtuhumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanajihusisha na tabia hiyo.

“Upande wa Jamhuri umetoa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kuingiliwa kinyume cha maumbile kwa kujitambua,”amesema.

Awali inadaiwa mtuhumiwa alisambaza picha za video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa amevalia mavazi ya kike huku akitembea usiku wa manane ambapo alikamatwa na sungusungu waliokuwa doria na kufikisha katika vyombo vya dola.

Mkazi wa Mikoroshini wilayani humo, Anna Sanga ameiomba jamii kuwafichua wanaume wenye tabia hizo chafu ili sheria ichukue mkondo wake kwani wamekuwa wachafua tamaduni za Kitanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top