JUMUIYA YA 'FARAJA YETU' YATOA FARAJA KWA FAMILIA 30 ZENYE WATOTO YATIMA CHAMBANI.

Hassan Msellem
0

Jumuiya ya Faraja Yetu Kisiwani Pemba imesema itashirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji wa futari huko katika Kijiji Cha Chwale Chambani, Makamo mwenyewekiti wa jumuiya ya Faraja Yetu Bi. Riziki Mohammed Ramadhan, jumuiya ya Faraja Yetu ni jumuiya ambayo imeanzishwa Kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi ikiwemo watoto yatima, wenye ulemavu na wajane.


Aidha Bi. Riziki amewataka wazazi na walezi kuongeza umakini wa kuwa karibu na watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji vinavyo onekana kukithiri.


Kwa upande wake mwalimu wa madrasa Ali Mohammed Khatib, ameziomba jumuiya nyengine kuiga mfano wa jumuiya hiyo ili kuwasaidia wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.


Nao baadhi ya wazazi na walezi wenye watoto yatima waliopatiwa msaada huo wameishukuru jumuiya hiyo Kwa kuwapatia msaada huo wa futari.

Jumla ya familia 30 zenye watoto yatima 102 kutoka Kijiji cha Chwale Chambani zimepatiwa msaada wa unga wa ngano na tende kutoka jumuiya ya Faraja Yetu.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top