JUMUIYA YA 'FARAJA YETU' YATOA MSAADA WA NGUO KWA AJILI YA SIKUKUU KAYA 100 ZENYE WATOTO YATIMA MICHEWENI.

Hassan Msellem
0

Wazazi na walezi wenye watoto yatima wametakiwa kuongeza umakini wa kuwa karibu na watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji vilivyokithiri hapa nchini.

Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa nguo kwa ajili ya sikukuu ya Iddi al-fitr huko Shumba Mjini Micheweni makamo mwenyewekiti wa jumuiya ya Faraja Yetu Bi. Riziki Mohammed Makame, amesema kutokana kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji nchini wazazi na walezi wanapaswa kuongeza umakini wa kuwa karibu na watoto ili kuwaepusha na vitendo hivyo.


Kwa upande wake mratib wa Faraja Yetu Suleiman Mahmoud Muhammad, amesema jukumu la kuzisaidia familia zenye watoto wenye mahitaji maalumu ni jukumu la kila mmoja ili kuzifariji familia hizo.


Nao baadhi ya wazazi na walezi wenye watoto yatima waliopatiwa msaada huo wa nguo wameishukuru jumuiya hiyo sambamba na kuziomba jumuiya nyengine kuiga mfano huo.


Jumla ya kaya 100 kutoka shehia ya Chamboni, Majenzi na zimepatiwa msaada huo Shumba Mjini Wilaya ya Micheweni zimepatiwa msaada wa nguo kwa ajili ya sikukuu ya Iddi al-fitr. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top