Kijana aliyebaka mtoto jela miaka 30

0

 Mkazi wa Kijiji cha Nyamigota, wilayani Geita mkoani hapa, Bahati Wilson (42) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwenda jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 12 (jina linahifadhiwa) mkazi wa kijijini hapo.


Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita, Nyakato Bigirwa amesoma hukumu ya kesi hiyo namba 177 ya mwaka 2022 baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia.

Awali Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri, Boniface Mwondo alieleza kuwa Bahati alitenda kosa hilo Julai 18, mwaka jana kinyume na kifungu cha 130 (1) na (2)e na kifungu cha 131 (1) cha sheria ya kanuni za adhabu.

Mwondo alieleza kuwa baada ya kosa hilo askari wa sungusungu wa Kijiji cha Chibingo walimkamata mshitakiwa na Julai 19, mwaka jana na kuchukuliwa na askari polisi wa kituo kidogo cha Katoro kwa mahojiano.

Aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa alihojiwa na askari polisi kituo kidogo Katoro na kukiri kutenda kosa hilo na Septemba 13, mwaka jana alifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka.

Alisema mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na kudai maelezo ya awali ya kukiri kosa hilo Kituo Kidogo cha Polisi Katoro ni kwa sababu aliogopa vitisho.

Aidha, Machi 20, mwaka huu mshitakiwa alisomewa mashitaka na kukutwa na kesi ya kujibu na kuhojiwa iwapo ana utetezi, mtuhumiwa alieleza hana utetezi na kuruhusu mahakama iamue itakavyoona.

Mbali na kukosa utetezi mshitakiwa aliomba kubadilishiwa hakimu kwa sababu ya mashaka kwamba huenda asingetendewa haki.

Madai ya kwanza ya mshitakiwa ni kupokea vitisho kutokana na maagizo ya hakimu, pili kunyimwa haki za msingi za kuwahoji mashahidi na tatu ni hakimu kuegemea upande wa Jamhuri.
Mahakama ilitupilia mbali madai ya mshitakiwa na kwa kuzingatia hoja za mashahidi sita na vielelezo vinane alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top