Kilio cha wananchi wa Ntevele Makete kuchota maji mtoni sasa kutafutiwa ufumbuzi..

0

 Wananchi wa kitongoji cha Ntevele kijiji cha Ng'onde wilayani Makete mkoani Njombe wapo mbioni kuondokana na kero ya muda mrefu ya kukosa huduma ya maji ya bomba


Katika kikao cha RUWASA wilaya ya Makete na wananchi hao, kilichoketi  Aprili 3,2023 imeelezwa kuwa tatizo hilo la maji litaanza kushughulikiwa kuanzia Aprili 4,2023 ambapo kazi ya kwanza itakuwa ni kuchimba mitaro na kufukia mabomba kisha hatua nyingine zifuate

Hizo ni taarifa njema kwa wananchi wa kitongoji hicho ambapo awali walizielekeza lawama kwa diwani wao wakimtuhumu kuhusika kuchimba mabomba yaliyokuwa yakiwapelekea maji kama alivyoeleza mkazi wa kitongoji hicho Jeina Mbogela katika mahojiano maalum na Green FM

"Naishukuru serikali ya Rais Samia imesikia kilio chetu, tulikuwa tunachota maji mtoni, na hata vyoo vya kuflash tulivifunga kutokana na kukosa maji, lakini tunawashukuru viongozi wetu wamelishughulikia hili, asanteni sana" amesema Mbogela

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Kombolewa Malila amesema wao wapo tayari kutoa ushirikiano ili mradi huo ukamilike kwa wakati

Diwani wa kata ya Mlondwe Alphonce Salimo ambapo kitongoji hicho kipo, amekanusha tuhuma za yeye kung'oa mabomba na kusema hayo yalikuwa maamuzi ya wananchi walioamua mabomba hayo yafukuliwe na kutumika kwenye kitongoji kingine chenye watu wengi huku akiishukuru serikali kwa kuwapatia fedha za kutatua changamoto hiyo ya maji

Diwani huyo amewataka wananchi kupuuza taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa mitandaoni zikimtuhumu kuhujumu mradi wa awali wa maji katika kitongoji hicho
Meneja wa RUWASA wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesema kwa sasa utekelezaji wa zoezi hilo unaendelea ambapo serikali ilitoa shilingi milioni 100 na wanatarajia ndani ya kipindi cha mwezi mmoja watamaliza kazi hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top