Mwenge wa Uhuru Aprili 27, 2023 umetembelea miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 katika halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe
Ukiwa katika kata ya Tandala umetembelea kikundi cha bodaboda kilichopatiwa mkopo wa pikipiki na halmashauri ya wilaya ya Makete, kikundi hicho kupitia kwa msoma taarifa kimeelezea hatua walipofikia sasa tangu kukabidhiwa pikipiki hizo na mbio za mwenge wa uhuru mwaka jana, ambapo wamesema wanaendelea kurejesha mkopo huo na wapo waliofanikiwa kujenga nyumba
Akikagua mradi huo licha ya kuwapongeza uendelevu wake ikiwemo kufanya marejesho kwa wakati, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdalla Shaibu Kaim ameelezea dosari walizozigudua katika kikundi hicho ikiwemo madereva kukosa vyeti vya mafunzo, pikipiki kukosa sight mirror pamoja na baadhi yao kutokuwa na elimu ya sheria za barabarani baada ya kushindwa kujibu maswali waliyowauliza
Ndipo Kiongozi huyo akatoa maagizo yanayotakiwa kutekelezwa ndani ya siku 14 kwamba pikipiki za kikundi hicho zikabidhiwe kwa mkuu wa polisi wilaya ya Makete hadi wapatiwe mafunzo na taarifa waipate ndipo wakabidhiwe pikipiki zao
Mwenge huo umeendeleza mbio zake ukitokea wilaya ya Njombe ambapo ukiwa wilayani hapo umekimbizwa Zaidi ya kilomita 112 na kupitia miradi iliyopo katika kata ya Mang’oto, Tandala, Lupalilo na Iwawa.