Kiongozi wa soko atokomea na malipo ya Kodi za vibanda vya biashara

0

 Wafanyabiashara wa soko la Igawilo Jiji Mbeya Mkoa wa Mbeya walia na mstaafu aliyekuwa Mkuu wa soko hilo kwa kukusanya kodi ya vibanda vya biashara vya Jiji hilo na kutokomea kusikojulikana.


Wafanyabiashara wa soko hilo walikuja kubaini wameibiwa baada ya ofisi ya Mkurugenzi kuja kukusanya Malipo ya vibanda hivyo ndipo walipohoji tulishalipa kwa Mkuu wa Soko kumbe tayari alikuwa mstaafu.

Nae Bi Merry Joseph Ambae ni kaimu mkurugenzi wa Jiji amesema taarifa za wao kulipa hela kwa mstaafu huyo tayari wanazo, wanachopaswa kufanya wafanyabiashara ni kumshitaki mtu huyo aliyekuwa anakabidhiwa fedha hizo .

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya wa Mbeya Beno Malisa ameiagiza ofisi yake kufanya mazungumzo na wafanya biashara hao Ili kutatua changamoto hiyo na kuwapa elimu wafanyabiashara hao kuwa kwa Sasa Malipo yote ya serikali yanafanywa kwa njia ya bank na sio mkononi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top