Mwanamke mmoja kutoka nchini Nigeria amejaliwa kujifungua watoto watano mapacha baada ya miaka tisa ya kusubiri kuitwa mama.
Chidimma Amaechi, na mumewe ambao wamekuwa katika ndoa kwa miaka tisa, bila mtoto, hatimaye wametembelewa na Mungu wa Abrahamu na Sarah ambaye amewafuta machozi kwa kuwapa zawadi ya malaika watano.
Watoto hao watano ni pamoja na wavulana watatu na wasichana wawili waliozaliwa mnamo Alhamisi, Machi 30 2023.
Jamaa na marafiki wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuwapongeza wanandoa hao huku wakimsifu Mwenyezi Mungu kwa baraka hizo.
Nnamani Nicky Ginika aliandika: “Hongera sana Chidimma Amaechi. Bwana amekurehemu baada ya miaka 9 ya kuvumilia,Kwa kila mwanamke anayemtumaini Mungu kwa tunda la tumbo..Bwana atakukumbuka kwa njia hii..Amina”.
Onyinye Peace: "Chidimma Amaechi. Miaka 9 ya kusubiri. Miaka 9 ya kuchelewa. Miaka 9 ya kulia. Miaka 9 ya kukosa usingizi. Miaka 9 ya kejeli. Miaka 9 ya aibu iliisha. Kwa wote wanaongojea mama wa Mungu aliyeondoa aibu yangu atawatembelea na kuwapa baraka za namna hii.”