Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamtafuta Mariamu Salumu mkazi wa Kisesa mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kutelekeza watoto wake wawili wenye umri chini ya miaka 18 na kusababisha kuishi katika mazingira hatarishi huku likimshikilia James Julius mkazi wa Kahama kwa kuishi na watoto hao kinyume cha sheria.Picha kutoka maktaba haihusiani na habari hii
Wasafi Media imefika hadi mtaa wa Majengo ndani ya manispaa ya kahama na kuzungumza na mmoja watoto waliotelekezwa kwa zaidi ya miezi miwili licha ya kuwa na umri wa 17 binti huyu ambaye alikatishwa masomo akiwa darasa la tatu na kulazimika kufanya kazi za ndani ili akimtunza mdogo wake wa miaka 2.
Mkazi wa kahama Shasta karina ameelezea namna watoto hao walivyofika Kahama huku Anascholastica Ndagiwe mdau wa kupinga vitendo vya ukatili kutoka Taasisi ya Wanawake laki moja mkoa wa Shinyanga ameeleza namna walivyowanusuru watoto hao na janga la ukatili.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kumshikiria kijana aliyewasafirisha na kutoa rai kwa wazazi kuwajibika kwenye malezi.