Mbakaji wa Facebook akamatwa Tanzania

0

Jeshi la Polisi Tanzania jioni ya april 8.2023 limethibitisha kuwa Makachero wa Tanzania wamewakamata Raia watatu wa Afrika Kusini ambao ni Thabo Bester maarufu kwa jina la ‘Mbakaji wa Facebook’, Mpenzi wake Dr. Nandipa Magumana na Zakaria Alberto.

Mtuhumiwa

Inadaiwa watatu hao wamekamatiwa Arusha japo taarifa rasmi yaPolisi haijasema eneo walikokamatiwa, kwa upande mwingine Msemaji wa Polisi Makao Makuu David Misime amesema taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya kimataifa zinaendelea kukamilishwa.

Itakumbukwa kuwa Thabo amekuwa akisakwa na Polisi wa Afrika Kusini akikabiliwa na kosa la kughushi kuwa amefariki alipokuwa gerezani na kutoroka kisha baadaye ikabainika kuwa hajafariki, kitendo ambacho kiliishangaza Nchi nzima.

Mamlaka iliamini kuwa Thabo Bester alifariki baada ya kujichoma moto katika Gereza la Hloko Jijini Bloemfontein May 2022 lakini baadaye ikabainika mwili uliodaiwa ni wa Thabo haukuwa wake ambapo mwanzoni mwa mwezi huu Polisi Afrika Kusini walianzisha msako mkali wa kumtafuta.

Thabo alidaiwa kuwarubuni Waathiriwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kisha kuwabaka na kuwaibia ambapo mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji, wizi na mauaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top