Mbunge Kishimba ataka ianzishwe wizara ya Kero Tanzania

0

 Mbunge wa Kahama Mjini, Jumanne Kishimba ameiomba Serikali kuanzisha Wizara mpya zitakazoshughulika na kero mbalimbali na nyingine kuyatazama matumizi ya Serikali ambapo ameshauri ziitwe Wizara ya Kero na nyingine Wizara ya Matumizu ili kupunguza upotevu wa fedha za Serikali.

Jumanne Kishimba

Kishimba ameyasema hayo Bungeni Dodoma April 12, 2023 ambapo ameainisha kero mbalimbali ambazo anasema hajui pa kuzipeleka lakini kukiwa na Wizara hiyo itazipokea na kuzifikisha panapohusika, aidha Kishimba amesema suala la kujadili ripoti ya CAG wakati hela zimeshaliwa haina msaada hivyo ameshauri ni kuwepo na Wizara ya matumizi ambayo itaifanyia tathmini miradi mbalimbali kabla ya kutekelezwa.

“Kwanini CAG anakagua baada ya tukio, kwanini asianze kabla ya mradi, kawaida mbwa huwa anabweka wakati kuna mwizi ili mwenye mali atoke lakini mbwa akibweka baada ya kuibiwa inawezekana mbwa hakuwepo kwenye eneo lile kwa hiyo tuombe kama itakupendeza tuwe na Wizara ya Matumizu na Wizara ya Kero”

“Mfano unajenga soko la ghorofa na unatumia Tsh. Bilioni 30 unaweka nyanya na samaki halafu unategemea Watu waende kununua pale lakini tukiwa na Wizara ya Matumizi huu mradi ungepelekwa kwao wakauangalia kama unafaa ili wawapelekee TAKUKURU na CAG ndio uje Bungeni ili tukianza kuzozana hapa pesa hazijaenda lakini hapa sasa tunazozana pesa zimeenda”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top