Mhubiri huyo anayezingirwa na utata, huwaburudisha waumini wake kila anapopanda kwenye mimbari. Video imeibuka ya pasta huyo na waumini wake wakiimba wimbo na kucheza densi kabla ya Ng'ang'a kuwaelekeza kondoo wake kuruka kama vyura na kupiga 'push-ups'.
Ng'ang'a aliongoza waumini kufanya mazoezi huku muziki ukipiga kwa sauti ya juu.
Kuanzia wapokezi wa wageni hadi wahuudmu wengine, kila mtu aliburudishwa na kupata muda wa kufanya mazoezi.
Video hiyo imezua hisia tofauti mtandaoni, huku wengi wakieleza hamu yao ya kuhudhuria ibada za Jumapili katika kanisa hilo lenye makao yake makuu CBD.