Mume Afariki baada ya mke wake kumrusha kutoka ghorofani

0

 Mwanamume mmoja katika eneo la Ruaraka kaunti ya Nairobi amefariki baada ya mpenzi wake kumsukuma na kumuangusha kutoka ghorofani.

Braiton Litoro alifariki katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta alipokuwa akipokea matibabu baada ya mkewe Celestine Adhiambo kumpiga kabla ya kumuangusha kutoka juu ya ghorofa walimokuwa wakiishi.

Tukio hilo lilitokea mnamo Ijumaa Machi 31.2023

Adhiambo mwenye umri wa miaka 36 sasa anatarajiwa kufunguliwa mashataki ya mauaji baada ya mumewe kufariki alipokuwa akipokea matibabu.

Alitakiwa kushtakiwa kwa kosa la kujaribu kusababisha kifo cha Litoro kinyume cha sheria kwa kumshambulia vibaya.

Bi Oyeko ataendelea kushikiliwa na polisi hadi Aprili 5 atakapofunguliwa mashtaka ya mauaji katika mahakama kuu jijini Nairobi.

Bi Oyeko alikuwa ameamua kukatisha uhusiano wake na Litoro na kumfahamisha kabla ya kubadilisha kufuli katika nyumba yao.

Kabla ya kumuua mumewe alimwambia asilipe tena kodi ya nyumba kwani hataki kuishi naye.

Bi Oyeko alikuwa amerejea nyumbani na mpenzi wake mpya na kumpata Litoro katika nyumba isiyo na watu baada ya kurejea nyumbani mwendo wa saa tano usiku.

Wapenzi hao wawili wapya wanasemekana kumvamia kwa pamoja na kumsababishia majeraha mabaya kabla ya kumtupa chini mumewe.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top