Mkurugenzi Jinsia, awakunga Vijana juu ya dawa za kulevya na udhalilishaji Pemba.

Hassan Msellem
0

Vijana Kisiwani Pemba wametakiwa kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo ya udhalilishaji ili kutimiza ndoto zao walizojiwekea.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto Bi. Siti Abass Ali, wakati akizungumza na wananchi katika maeneo tofauti wakiwemo Vijana wa Jeshi la kujenga Uchumi JKU kanda ya Pemba, katika ziara yake aliyoifanya kisiwani humo yenye lengo la kutoa elimu ya kujikinga na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na udhalilishaji.


Amesema vijana wengi hivi sasa wamejiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya na udhalilishaji jambo linalopelekea kukatisha ndoto zao walizojiwekea.


Aidha mkurugenzi huyo amewaasa vijana wakike kujitambua na kujithamini kwani wao ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa vitendo vya udhalilishaji.


Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Kambi ya Msaani Wete Meja Ramadhani Mohd Abdalla, amesema wataifanyia kazi elimu hiyo na kuifanya kama somo la maalumu la kuwafundisha Vijana hao.


Katika ziara yake hiyo amezungumza na makundi mbali mbali wakiwemo wazazi, vijana wa jeshi la kujenga uchumi JKU Pamoja na wanafunzi wa Almadrasi Islamia iliyopo Vikunguni Kisiwani Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top