MOTO ATTEKETEZA BWENI LA WANAFUNZI VWAWA MKOANI SONGWE LEO

0

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeunguza bweni la Wanafunzi 64 katika Shule ya Sekondari Vwawa iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Songwe, Elautery Mremi amesema moto huo umeanza Ijumaa Aprili 14, 2023 asubuhi ambapo Jeshi hilo limefanikiwa kuudhibiti usienee kwenye mabweni mengine na madarasa.

Kamanda huyo amesema kuwa hakuna majeraha wala vifo vilivyosababishwa na moto huo huku tathmini ikiendelea kubaini madhara na chanzo cha moto huo.

Kamanda Mremi amesema bweni hilo lilikuwa linatumiwa na Wanafunzi 64 ambapo vitu vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo vimeteketea, wakati moto huo unatokea Wanafunzi walikuwa darasani wakiendelea na mitihani.

Kamanda Mremi amesema changamoto iliyotokea ni Jeshi hilo kupata taarifa kwa kuchelewa huku akitoa wito kwa Uongozi wa Shule ambazo zina mabweni kuweka Walinzi muda wote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top