Mpina ataka Mwigulu na Mbarawa wakamatwe, washtakiwe kwa uhujumu uchumi

0

 Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amesema kutokana na madudu yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu mradi wa reli ya kisasa SGR- Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa wanapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa uhujumu uchumi.

Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukataa nchi kuigeuzwa kuwa ‘shamba la bibi’.

“Na mimi nasema mawaziri, watendaji wote wa serikali waliohusika na watendaji mapema iwezekanavyo wakamatwe, washtakiwe na wafunguliwe makosa ya uhujumu wa nchi,” amesema Mpina.

Mpina ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Aprili 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya ofisi ya waziri mkuu.

Amesema kwa uchambuzi alioufanya katika ripoti ya CAG, kuhusu ubadhirifu uliotendeka, ni kwamba jumla ya Sh trilioni 30 zimetafunwa.

Mpina alianza kwa kubainisha namna Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) ulivyoshindwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara licha ya Bunge kutenga fedha za kutosha.

“Jumla ya Sh trilioni 3.14 hazikutumika ikiwamo Sh trilioni 2.9 fedha zilizotengwa kwa Tanroad ili watanzania wajengewe barabara. Lakini zaidi ya trilioni 2.9 hazikwenda kufanya kazi,” amesema.

Aidha, amesema ripoti hiyo ya CAG imebainisha namna sheria ya manunuzi haikufuatwa.

“Nilisimama nikazungumzia juu Lot namba 6 katika mradi wa SGR kutoka Tabora kwenye Kigoma, kwamba TRC imeacha bei ya ushindani kwa Kilomita ya SGR ya bilioni 9.1 imeenda kumpa mkandarasi CCECC kwa Sh bilioni 12.5, yaani ni zaidi ya Sh bilioni 3.4 kwa kilomita na kuisababishia hasara Sh trilioni 1.7 wakati mkataba unaendelea.  Tusipoingilia kati utaendelea na nchi imekula hasara.

“Katika lot 3,4 Mkaguzi amethibitisha kwamba tumepunjwa trilioni 1.7, lakini pia ununuzi wa mabehewa bilioni 503 jumla trilioni 4 jumla zimetumika,” amesema.

Amesema waziri wa fedha na mipango Dk. Mwigulu Nchemba alienda kukopa kwa sharti la kuvunja sheria ya manunuzi ambayo hana uwezo.

“Hana uwezo kisheria na kikatiba lakini mpaka sasa waziri wa fedha, wa uchukuzi, mkurugenzi wa TRC sijui kwanini hawajakamatwa na kufunguliwa makosa ya uhujumu uchumi… mpaka sasa hivi wako hapa.

“Waziri wa fedha ameenda kukopa trilioni 1.285 bila ridhaa ya bunge wala mtu yeyote. Hatujui zimeenda kufanya nini au amezipeleka wapi na linaendelea kutunzwa kwa usiri mkubwa,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top