Mtoto afariki kwa kuchapwa na baba yake baada ya kumkuta akijiandaa kunajisiwa na babu yake

0

JESHI la Polisi Mkoa wa mwanza limesema linamshikilia baba kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wake wa miaka 11 baada ya kukutwa bafuni akijiandaa kunajisiwa na babu yake mdogo.


Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Wilbroad W. Mutafungwa- SACP imesema kuwa inadaiwa Tarehe Aprili 03, 2023 majira ya saa 12:00 mchana, kuliripotiwa tukio la mauaji ya Milembe Mihayo, miaka 11, mkazi Sumaha, baada kupigwa na baba yake mzazi siku ya tarehe 27.03.2023 majira ya saa 08:00 asubuhi katika kitongoji cha Ishungi kata ya Wala Wilayani Kwimba.


Baada ya kulipotiwa kwa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi lilifatilia kwa haraka na kufanikiwa kumkamata Mathayo Mishaka, miaka 40, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Sumaha.

 Baada ya mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na mauaji ya binti yake kwa kumchapa na fimbo sehemu za mwili wake baada ya kumkuta nyumbani kwa babu yake mdogo aitwaye Dotto Masanyiwa alikokuwa ameagizwa, wakiwa bafuni na mvulana aliye kimbia baada ya kufumaniwa wakiwa wamevua nguo wakitaka kufanya mapenzi ndipo alipomkamata binti yake na kuanza kumpiga.

Milembe Mihayo aliendelea kupata maumivu makali bila kupelekwa Hospitali, ndipo baba yake huyo mzazi akamuagiza mke wake mdogo aitwaye Sofia Mashaka, Miaka 20, amkande miguu binti huyo iliyokuwa imevimba kutokana na kipigo na mama huyo alipomuuliza mmewe kuhusu tatizo hilo, alimueleza kuwa binti huyo huwa anasumbuliwa na tatizo la miguu kitendo ambacho mama huyu hakulizika nacho kwani alikuwa ameishi na binti huyo kwa muda wa mwaka mmoja bila kuona tatizo hilo.

Mwili wa Milembe Mihayo umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya kukamilishwa kwa upelelezi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutoa adhabu za kikatili kwa watoto wao badalayake watumie njia sahii ya kuwaonya pindi wanapokose ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

 Pia, linawaomba kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top