Mtoto Ala Milioni 3.5 Zilizochangishwa Kusimamia Mazishi ya Mamake Mzazi

0

 

Joseph Oseko kutoka kaunti ya Nyamrira nchini Kenya anadaiwa kuchangisha kima cha shilingi milioni 3.5 ambazo zilitarajiwa kutumika katika mazishi ya mamake mzazi lakini badala yake akaamua kuzifyonza fedha hizo. 


Kulingana Diana Kerubo Oseko ambaye ni dadake Joseph ni kuwa kakake alichangisha fedha hizo na kisha kutoweka na kuuacha mwili wa mama yao ukisalia kwenye chumba cha wafu. "Pesa ambazo zilikusudiwa kutumika kwa shughuli ya mazishi zilielekezwa kwa matumizi ya kibinafsi na watoto wakasahau kuhusu mama yao na kumwacha aharibikie kwenye chumba cha maiti. 


Ukiona hali ya maiti ya Mama Yuniah ilivyo sasa utalia wiki nzima. Mwili hauko sawa kabisa. Hutatamani kumuona mama yako katika hali hii. Utaingiwa na huzuni mara moja," Kerubo alisema.


Kerubo amesema kuwa jamii inastahili kuingilia kati ili kuhakikisha kuwa mazishi ya mama yao yanafanyika kwani iwapo shughuli hiyo itawachwa mikononi mwa ndugu zake basi huwenda mama yao mzazi akakosa kuzikwa.


Sintofahamu Kati ya Mandugu Kerubo amesema kuwa kakake Joseph aliwazui na kutowahusisha katika shughuli za umiliki wa mali yao. Mwanadada huyo aliongeza kuwa mahakama iliamuru kuwa mama yao mzazi aweze kuzikwa sehemu alipozikwa baba yao. 


“Wakati jamaa na wanajamii wakijaribu kuandaa mazishi ya mama yetu alituma majambazi kwenda kuharibu maskani na kuwafukuza watu waliokuwa wakimuomboleza mama yetu mpendwa. Hatuhitaji msaada wowote wa fedha kwa sababu fedha zilizokusanywa kutoka kwa umma hazikutimiza malengo yake. 


Tunamtaka atoe pesa ambazo zilielekezwa kwa M-pesa yake au mali zake zitwaliwe ili kumwachilia mama yetu kutoka chumba cha maiti," Kerubo alisema. Joseph ameieleza TUKO.co.ke kuwa mzozo wa shamba unaoshuhudiwa ulianza kabla ya kifo cha mama yao na kuwa kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa kwa makachero wa DCI na marehemu mama yao.


Joseph amesema kuwa kwa fedha alizozipokea alitumia shilingi 900,000 kulipa bili ya hospitali na kusema kuwa bili ya kuuweka mwili katika chumba cha maiti japo imeongezeka italipwa wakati kesi iliyowasilishwa mahakamani itakamilishwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top