Mume na Mke watelekeza watoto watokomea kusiko julikana mkoani Arusha

0

 Wakazi wa Kata ya Muriet, eneo la Barabara ya Nado, mitaa ambayo ni maarufu kwa jina la Muriet au Barabara ya East Afrika Mkoani Arusha, wamelalamikia kitendo cha wazazi wawili (mume na mke) kuwatelekeza watoto wao ambao wamejikuta wakiingia katika matatizo ya kimaadili.

Picha kutoka Maktaba haihusiani na tukio halisi


Inaelezwa kuwa Wazazi hao ambao majina yao hayajapatikana walikuwa na mgogoro wa kifamilia, mume akaondoka lakini siku chache baadaye akarejea na wakakubaliana kuwa waendelee kulea Watoto hao licha ya tofauti zao binafsi.

Katika mazingira ambayo haijulikani nini kilitokea, mume alichukua maamuzi ya kuondoka na kutokomea kusikojulikana kisha siku chache baadaye mke naye akaondoka bila kuaga, hivyo wakawaacha watoto wao mmoja ambaye inadaiwa ana umri wa miaka 17, mwingine inadaiwa ana umri wa miaka 15 na wa mwisho ambaye inadaiwa ana umri wa miaka 6 au 7.

Mama wa Watoto akiwa mafichoni akawa anatuma hela kupitia kwa jirani yake ili awape wanaye kwa ajili ya matumizi ya chakula, baada ya siku kadhaa jirani huyo ambaye ni Mwanamke naye akakataa kupokea fedha hizo kwa kile kilichoelezwa kuwa anaogopa kuingia katika matatizo kwa kuonekana anaunga mkono kinachofanywa na mama Watoto aliyekimbia familia.

Wakati anaondoka mama mtu aliacha simu nyingine nyumbani kwake, ndipo akaendelea kuwasiliana nao kwa njia hiyo huku akiwatumia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya matumizi.

Licha ya kutoonekana wakienda shule, hivi karibuni majirani waliona yule mtoto mdogo akitembea kwa kuchechemea, baada ya kumuuliza tatizo lake akaogopa kusema akiwaambia ametishiwa na kaka zake kuwa akisema watamua.

Majirani wakatumia ushawishi mwingi azungumze, ndipo Mtoto huyo akafichua kuwa amekuwa akiingiliwa kinyume cha maumbile (analawitiwa) na kaka zake kwa zamu.

Kaka zake hao walipoitwa na kubanwa kuhusu kufanya vitendo hivyo wakakana kufanya matukio hayo huku wakionesha kutokuwa tayari kutoa ushirikiano wa kuulizwa maswali zaidi.

Ndipo Balozi wa Mtaa wa Muriet, Zuhura Ally Toto akashirikiana na wananchi wakampeleka Mtoto aliyeathiriwa na ukatili wa ndugu zake hospitali, madaktari wakakataa kutoa huduma hadi wapate PF3 kutoka Polisi.

Baada ya maombi ya Balozi ndipo madaktari wakamfanyia uchunguzi na ikabainika kweli mtoto huyo ameingiliwa, wakasaidia kumpa dawa.

Akifafanua zaidi, Balozi wa Mtaa wa Muriet, Zuhura anasema “Hadi muda huu tunaye huyu mwathirika kwa kuwa tunajua tukimrudisha kule kwa wenzake wanaweza kumfanyia kitu kibaya zaidi, pia hata kiakiri ni wazi hayupo sawa.”

Anaongeza; “Tumewasiliana na mama Watoto amekataa kurudi kwa kuwa anadai tunamdanganya ili arudi kisha wanaomdai waweze kumkamata. Tangu tumpe hizo taarifa hapokei tena simu.”

Inadaiwa yule jirani wa awali aliyekuwa akitumiwa hela ili awape Watoto naye alipomjulisha mama mzazi kuhusu tukio la ulawiti, inadaiwa aligoma kurudi kwa kuamini kuwa wanamdanganya ili akirudi akamatwe na wadeni wake.

Kuhusu madeni, inaelezwa kuwa kutokana na madeni ambayo mama huyo anadaiwa, baadhi ya wanaomdai walifika nyumbani kwake na kubeba baadhi ya vitu ikiwemo kitanda, hivyo Watoto hao wamekuwa wakilala chini.

Balozi Zuhura anasema; “Tunawasiliana na Mwenyekiti wa Mtaa ili kulifikisha suala hili mbele zaidi kwenye vyombo husika kwa kuwa hakuna ushirikiano kutoka kwa wazazi na hata afya ya akili ya Watoto husika inaonekana haipo sawa.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top