Mwalimu wa 'tuition' asakwa akidaiwa kulawiti

0

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani hapa kumsaka na kumkamata mwalimu (jina halijatajwa) kwa madai ya kumlawiti mmoja wa wanafunzi wake waliokuwa wakisoma masomo ya ziada (twisheni) kwake.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Batilda Buriani,

Dk. Buriani amesema mwalimu huyo anadaiwa baada ya kufanya kitendo hicho kwa mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma moja ya shule zilizoko Manispaa ya Tabora, amekimbia.

Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini na serikali mkoani hapa wakati wa hafla fupi ya kufuturisha iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Alisema serikali hawezi kuendelea kuvumilia vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu.

Dk. Buriani alisema hivi karibuni akiwa kwenye shughuli za Bunge jijini Dodoma, alipokea taarifa za tukio la mwalimu huyo ambaye wazazi na walezi walimwamini na kumkabidhi watoto wa darasa la tatu na la nne ili awafundishe masomo ya ziada,

Alisema wanafunzi wakienda kusoma masomo hayo, baadhi yao walikuwa wakipewa kazi na kutoka nje na kubaki na mwanafunzi huyo na kumfanyia kitendo hicho.

Wazazi wa mtoto huyo, alisema waligundua kuwapo kwa tabia hiyo baada ya mwanafunzi huyo kukataa kwenda shule na walipomwadhibu ndipo akaeleza vitendo anavyofanyiwa na mwalimu huyo.

“Kwa kweli tukio hili limenisikitisha sana. Mtoto alifanyiwa vipimo na kukutwa ni kweli ametendewa hivyo. Kesi iko polisi inakwenda mahakamani licha ya mwalimu huyu kukimbia. Ninaagiza atafutwe na kukamatwa haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza.

Dk. Buriani alisema wamepanga kuendelea kukagua vituo vya kulelea watoto yatima na kupita shuleni mara kwa mara kwa kushirikisha viongozi ngazi za vijiji.

Sheikh wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Tabora, Ibrahimu Mavumbi, amewataka viongozi wa dini kuendelea kukemea ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ya ibada na kudhibiti viashiria vya ndoa za jinsia moja kwa kuwa, jambo hilo halimpendezi Mungu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top