Mwanamke Anusurika kuuawa akituhumiwa kuiba kisa kumkataa mwanaume

0

 Mwanamke mmoja aitwaye Manka Mushi (26) mkazi wa Ikoma Kata ya Itilima Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga amenusurika kifo baada ya kupigwa na jeshi la jadi (Sungusungu) kwa tuhuma za wizi wa shilingi laki nne na elfu 20 za Kitanzania.


Akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga alipolazwa kwa ajili ya Matibabu, Manka amesema madhila hayo yalimkuta mnamo Aprili 14, 2023 usiku baada ya kumkataa mwanaume aliyekuwa akimtaka kimapenzi ndipo akasema kuwa amemuibia pesa hiyo.

Amesema baada ya tukio hilo mwanaume huyo alimshika kwa nguvu na kumtishia kumuua kwa kumnyonga shingo hadi haja kubwa ikatoka kisha kumfikisha kwa sungusungu ili aadhibiwe ambapo aliadhibiwa viboko vilivyochangia kupoteza fahamu.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Prisila Mushi amesema Manka alipokelewa akiwa na hali mbaya na kwamba baada ya matibabu anaendelea vema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top