Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mwanaume ambaye hajatambulika,kasha mwili wake kutelekezwa pembezoni mwa kilabu cha pombe kilichopo mtaa wa misheni wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza
Mauaji hayo yanadaiwa kutokea usiku wa kuamkia 13 April 2023 ambapo mwili wake umekutwa na majeraha usoni na sehemu za siri zikiwa zimetobolewa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema wanaoshikiliwa ni pamoja na mmiliki wa kilabu hicho cha pombe za kienyeji.
Mwili huo ulikuwa umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utambuzi.