Mwanahabari Maynard Manyowa kutoka nchini Kenya kupitia mtandao wa kijamii amefichua kuwa kosa lake kubwa maishani ni kuoa wake wawili.
Mwanamume huyo ambaye
alijieleza kama mwanamume aliyekuwa na wake wengi, alikuwa akimjibu
swali kutoka kwa wafuasi katika ukurasa wake kwenye Twitter ambaye alipendekeza kuwa ndoa ya mitala ndio bora
zaidi
Alieleza kuwa
anapinga ndoa ya wake wengi kwa sababu ya uzoefu wake binafsi na wake zake
wawili, na akawataka wanaume waache mitala la sivyo hawatakuwa na amani katika
maisha yao.
Kulingana na Maynard,
anampenda mke wake wa kwanza na alimuoa mke wake wa pili ili kumwokoa kutoka
kwa aibu ya kuwa mseja.
Hata hivyo, baada ya
muda, alikaribia kumpoteza mke wake wa kwanza ambaye alimpenda sana kwa sababu
alitaka kubaki na mke wake wa pili.
"Kama mtu aliyekuwa katika ndoa ya mitala, nasema huu ni ushauri mbaya. Huwezi kuwa na amani kamwe katika maisha yako.
Nilikuwa na mke zaidi
ya mmoja kwa sababu niliwahi kumpenda mwanamke mmoja tu.
Na mwingine hakuwa Bibi wangu rasmi bali ni mtu ambaye sikutaka ateseke kwa sababu ya kutoolewa "Kosa kubwa zaidi kuwahi kutokea.