Mwl adaiwa kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu.

1

  Baada ya kusambaa video mtandaoni, akimuonesha mtoto darasa la tatu akisimulia namna alivyofanyiwa ukatili na mwalimu wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amesema hatua zimeshachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.

Picha kutoka mtandaoni haihusiani na tukio halisi

Dk Gwajima  ametoa majibu kupitia  mtandao wake wa kijamii wa Twitter,akiandika "shtaka la mtuhumiwa lipo polisi RB namba ARS/RB/3429/2023. Wako watoa  huduma ambao wamevaa vazi la kondoo kumbe ni wanyama wakali dhidi ya watoto .


Wazazi semeni na watoto msisubiri tukio limkute, semanae sasahivi hapo ulipo 'mwanangu marufuku mtu kuleta agenda za kugusa mwili wako wala kupita pembeni na kukueleza lolote kukuambia usiseme wala asikutishe ukanyamaza piga kelele toa taarifa'"aliandika.

Hata hivyo katika maelezo yake amependekeza mbinu mpya kwa jamii, watoto kuwa na filimbi wakiona dalili za hatari ya mtu kutaka kushika mwili wake wapulize, kama mkakati moja wapo wa kukabiliana na vitendo hivyo.

Kwa uchache katika video hiyo, mtoto huyo ameeleza kuwa ameshawahi kulawitiwa  kwa zaidi ya mara tatu na mwalimu huyo.

Katika video hiyo inayosambaa mtandaoni mama mtoto huyo ameonekana akisimulia maswahibu yaliyompata mwanaye huyo akiiomba Serikali ichukue hatua kwa mhusika

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera kwa habari nzuri na zawakati katika blog yako.

    ReplyDelete
Post a Comment

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top